11.8 C
New York

Ahmed Ally: Simba itatinga robo fainali CAF

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini

BADO Simba ina nafasi ya kushinda mechi zilizobaki na kuingia robo fainali ya msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ahmed Ally.
Simba imepoteza mechi zote mbili za awali za Kundi D baada ya kufungwa na Petro de Atletico (1-0) na Stade Malien (2-1).

Ni kwa maana hiyo, ‘Wekundu wa Msimbazi’ wamebakiza mechi nne dhidi ya Malien (nyumbani), Atletico (ugenini) na Esperance de Tunis (nyumbani na ugenini).

Licha ya ugumu unaoonekana, Ally anaamini kikosi chao kina wachezaji wenye ubora wa kuwavusha hatua hii ya makundi msimu huu wa 2025-26. “Kama tutakaa na wachezaji, tukawapa moyo, naamini bado tuna nafasi ya kusonga mbele na kuingia robo fainali,” alisema Ally.

“Tunaweza kuifunga Malien hapa nyumbani, tunaweza kuifunga Petro (Atletico) kule kwao, pia tuna uwezo wa kushinda nyumbani na ugenini dhidi ya Esperance.”

Ally ameyasema hayo wakati huu Simba ikiwa haina kocha mkuu baada ya kumfungashia virago Dimitar Pantev. Pantev ameoneshwa mlango wa kutokea akiwa ameliongoza benchi la ufundi katika mechi nne za kimatafa (Ligi ya Mabingwa Afrika).

Katika michezo hiyo, Simba imeshinda mmoja (3-0 dhidi ya Nsingizini), imefungwa miwili na kutoa sare moja.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img