19.7 C
New York

Mtangazaji ahukumiwa kifo kisa dawa za kulevya

Published:

CAIRO, Misri

MTANGAZAJI maarufu wa vipindi vya televisheni nchini Misri, Sarah Khalifa, ni miongoni mwa watuhumiwa 11 walihukumiwa kifo kwa makosa ya kujihusisha na mtandao wa dawa za kulevya.

Katika taarifa yake, Gazeti la al-Ahram linalomilikiwa na Serikali, limedai kuwa Sarah na wenzake waliagiza na hatimaye kungiza nchini Misri vichanganyio vya kutengeneza dawa hivyo.

Wakati huo huo, mbali na hilo, pia walishitakiwa kwa kumiliki bunduki na vilipuzi kinyume cha wheria.

Sarah (39), anafahamika kupitia kipindi chake cha televisheni cha ‘Mission Impossible’ ambacho kinajihusisha na masuala ya uhalifu.

Hata hivyo, bibiye huyo amekana mashitaka yote dhidi yake, pia wanasheria wake wakisema wataikatia rufaa hukumu hiyo.

Related articles

Recent articles