JAKARTA, Indonesia
MLIPUKO wa Volcano katika Mlima Anak Krakatau umesababisha kusitishwa kwa safari za ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno-Hatta mjini Jakarta, Indonesia.
Kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka, mlipuko huo umezuia safari 209, hivyo kuathiri abiria zaidi ya 22,000.
Katika taarifa yake, Wizara ya Usafirishaji imeeleza kuwa baadhi ya safari zilizokwama ni pamoja na ya kwenda au kutoka Singapore.
Wakati huo huo, Wizara ilieleza kwamba safari zingine zilizoathiriwa ni zile za Doha, Sydney na Kuala Lumpur.
Aidha, Gazeti la Kompas la Indonesia limeripoti kuwa tukio hilo limesababisha kufungwa kwa shule na baadhi ya shughuli.


