24 C
New York

Mke wa Beckham ‘alivyotusua’ tasnia ya urembo

Published:

LOS ANGELES, Marekani

HIVI karibuni, mke wa David Beckham, Victoria, alitangaza faida ya Pauni milioni 7.3 kupitia kampuni yake ya mitindo na urembo, ambapo mauzo yameongezeka kwa
asilimia 15.

Hata hivyo, wengi watakumbuka kuwa haikuwa rahisi kufika hapo. Kwa ufupi, imechukua miaka 18 kwa ‘Posh’ kuanza kuiona faida ya kampuni yake hiyo.

Katika moja ya mahojiano yake, mwanamuziki huyo wa zamani wa Pop aliwahi kusema kampuni hiyo iliwahi kumuumiza kichwa kiasi cha kujuta kuianzisha.

Ni kwa namna kampuni ilivyokuwa ikitafuna pesa, ikiwamo bajeti ya Pauni 70,000 kila mwaka kwa ajili ya kununua maua tu. Wakati huo alikuwa akijihusisha na mitindo pekee.

Anakiri kuwa wakati fulani alihisi kuvurugwa kutokana na wingi wa madeni aliyokuwa nayo kupitia kampuni hiyo. “Ilikuwa ni safari yenye ‘jehanamu’ ndani yake.

“Nilipoteza kila kitu na kilikuwa kipindi kibaya kweli kweli,” alisema na kuongeza: “Nilikuwan alia kila siku kabla ya kwenda kazini …” alisisitiza Victoria, maarufu pia kwa jina la Posh Spice.

Tofauti na alivyotarajia, kwamba angefanikiwa haraka kutokana na umaarufu wa familia yake, Victoria alikumbana na makali ya biashara na wakati mwingine alilazimika kumuomba Beckham amsaidie kiasi cha fedha.

Mwaka 2019, aliamua kutanua uwanja kwa kuanzisha bidhaa na huduma za urembo kupitia ‘Victoria Beckham Beauty’ na huo ndiyo ukawa mwanzo wa kuyaona mafanikio.

Kwa sasa, kampuni yake inaingiza fedha nyingi kupitia eneo hilo la urembo kuliko biashara ya mitindo. Miongoni mwa wateja wake wa mwanzo na bado wameendelea kuwa naye, iwe kwenye mitindo au urembo, ni mke wa rapa Jay Z, Beyonce.

Pia, amekuwa akivuna pesa nyingi kutoka kwa Malkia wa muziki wa Pop, Lady Gaga, na bibiye anayetokea familia maarufu ya Kardashian, Kendall Jenner.

Hata hivyo, ni ngumu kuyazungumzia mafanikio ya kampuni yake pasi na kuwataja wanawake kama Lisa Maynard-Atem. Bibiye huyo ndiye mshauri wake wa mikakati ya kibiashara.

Related articles

Recent articles