22.1 C
New York

Nani kumaliza vita vya Putin, Ukraine?

Published:

MOSCOW, Urusi

WAZIRI Mkuu wa India, Narendra Modi, amemshauri mshirika wake mkubwa, Vladimir Putin, kumaliza vita vinavyoendelea kati ya nchi yake ya Urusi na majirani zao wa Ulaya Mashariki, Ukraine.

“Kila siku inayotumika vitani hurudisha nyuma ubinadamu na kila hatua inayochukuliwa katika kulinda amani huongeza ubinadamu …,” alisema Modi mapema wiki hii.

Kauli ya Modi inakuja zikiwa ni wiki tano tu tangu Putin alipopewa ushauri kama huo na Rais wa Kazakhstan, Kassym-Jomart Tokayev, lakini aliupokea na kuachana nao.

Kwanini India inaiomba Urusi kuacha vita? Serikali ya Modi imekuwa ikipewa presha kubwa na mataifa ya Magharibi tangu vita hivyo vianze. Kwa Magharibi, India inapaswa kuchagua upande; kuunga mkono au kulaani vita.

Kwa upande wake, India haijaweka wazi msimamo wake, ikizingatiwa kuwa tayari Urusi imeshatengwa na kuwekewa vikwazo na mataifa ya Magharibi tangu ilipoivamia Ukraine miaka minne iliyopita.

Badala ya kuungana na Urusi, jambo ambalo litasababishiwa nayo iwekewe vikwazo, au kupinga vita na kuharibu ukaribu wake na Urusi, India imeendelea kutaja mazungumzo kama njia sahihi ya kujenga.

Hata hivyo, kwa mataifa mengi ya Magharibi, msimamo wa India bado hautoi picha ya kuchukia vita hivyo, na badala yake yanatamani kuona India ikitangaza chuki dhidi ya Urusi.

Lakini, Modi amekuwa na tahadhari kubwa ya kuharibu ukaribu wake na Urusi, ikizingatiwa kuwa uchumi wa India umekuwa ukitegemea kwa kiasi kikubwa nafuu ya bei ya mafuta kutoka Moscow.

India inafahamu kuwa ushirikiano na Urusi na China umekuwa na tija kubwa katika uchumi wake, hivyo ukosoaji ‘usio na staha’ juu ya wa vita vya Ukraine unaweza kuleta sura tofauti.

Kwa upande mwingine, Serikali ya India haitaki kupoteza ushirikiano wake wa kiuchumi na Marekani na mataifa ya Ulaya, ingawa Urusi haivutiwi sana na urafiki huo.

Kwanini Putin hataki kumaliza vita? Urusi inaamini bado iko kwenye njia nzuri ya kushinda vita, licha ya kwamba ni miaka minne na zaidi tangu ilipoanza kuishambulia Ukraine.

Mbaya zaidi, kwa sasa ardhi ya Urusi ndiyo inayoumia zaidi kwa kugeuka uwanja wa machafuko, tofauti na awali, ambapo vita vilipiganwa nchini Ukraine.

Mathalan, hivi karibuni, ndege zisizo na rubani za Ukraine zilishambulia viwanda vya mafuta vya Urusi na kusababisha adha kubwa ya uhaba wa nishati hiyo.

Related articles

Recent articles