LAGOS, Nigeria
KIKONGWE mwenye umri wa miaka 101, bi. Esther Ogunmabo, anashikiliwa na polisini nchini Nigeria kwa kosa la kuuza dawa za kulevya aina ya bangi.
Ogunmabo alikamatwa Jumamosi ya wiki iliyopita katika Jimbo la Ogun, Kusini-Magharibi mwa Nigeria, kwa mujibu wa Mamlaka ya Kuzuia Dawa za Kulevya (NDLEA).
Taarifa zinaeleza kuwa alikutwa akiwa na mzigo wenye uzito wa gramu 90, zikiwamo kete ndogondogo zilizokuwa zimeandaliwa kwa ajili ya kuuzwa.
Baada ya kuhojiwa, Ogunmabo alikiri ni biashara yake na amekuwa akiuza bangi kwa muda mrefu. Ameachiwa kwa dhamana.
Taarifa kutoka NDLEA zinaeleza kuwa bibi huyo amekuwa akishirikiana na binti yake anayeishi Lagos, ambaye ndiye anayemtumia mzigo kwa ajili ya kuuza mitaani.


