JERUSALEM, Israel
MAMLAKA za Israel zimepitisha utaratibu wa kutumia mamba katika magereza yake, lengo likiwa ni kudhibiti wafungwa wanaotaka kutoroka.
Awali, Waziri wa Ulinzi wa Israel, Itamar Ben-Gvir, aliwasilisha ombi la kutaka wadudu hao kutumika kwa ajili ya usalama magerezani.
Katika ombi lake, alilenga magereza yanayoshikilia wafungwa wa kivita kutoka Palestina.
Moja ya magereza yaliyolengwa ni Ketziot lililoko Kusini mwa Israel, ambalo linashikilia Wapalestina wengi.
Katika taarifa yake kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Ben-Gvir amewaonya wafungwa watakaojaribu kutoroka.
“Mnafikiria kujaribu kutoroka? Fikirieni tena,” aliandika Waziri huyo, akisindikiza ujumbe huo na picha inayomuonesha akiwa na mamba.


