23.6 C
New York

Safari ya Argentina kutinga fainali

Published:

MIAMI, Argentina

ARGENTINA ya kocha Lionel Scaloni itaingia katika mchezo huo wa fainali dhidi ya Hispania ikiwa bingwa mtetezi kwa taji lake la miaka minne iliyopita nchini Qatar.

Vijana hao wa Kusini mwa Amerika wanasaka rekodi ya kuwa timu ya pili kutetea ubingwa wa Kombe la Dunia baada ya Brazil kufanya hivyo mwaka 1962.

Safari hii, ‘La Albiceleste’ walifuzu wakiwa kileleni mwa msimamo wa CONMEBOL (Shirikisho la Soka Kusini mwa Amerika).

Wakiwa Kundi J, vijana wa Scaloni walishinda mabao 3-0 katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Algeria. Messi alifunga ‘hat-trick’ siku hiy0.

Katika mchezo wao wa pili, waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Austria, kisha kuvuka hatua ya makundi kwa kuitandika Jordan mabao 3-1, siku ambayo Messi alitokea benchi na kufunga moja.
Walipoingia hatua ya 32 Bora, walikutana na Cape Verde, mchezo uliofika dakika 120 na Argentina kuibuka na ushindi wa mbinde wa mabao 3-2.

Hatua iliyofuata ya 16 Bora iliwakutanisha na Misri mjini Atlanta. Ni katika mchezo ambao Misri walitangulia kwa mabao 2-0, kabla ya Argentina kupindua meza na kushinda 3-2.

Ni baada ya ushindi huo, Argetina ikakutana na Uswis katika hatua ya robo fainali. Ni mchezo ambao Argentina ilizinduka dakika za jioni na kuondoka na ushindi wa mabao 3-1.

Baada ya mchezo huo, wakakutana na England katika mchezo wa hatua ya nusu fainali, ambapo waliweza kupata ushindi wa mabao 2-1, licha ya wapinzani wao hao kutangulia kuziona nyavu.

Kuelekea mchezo wa fainali, Messi ana mabao nane msimu huu wa Kombe la Dunia. Kwa jumla, staa huyo amefikisha mabao 21 katika historia ya michuano hiyo ya FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa).

Related articles

Recent articles