23.6 C
New York

Mechi 10 za kiume Kombe la Dunia 2026

Published:

BOSTON, Marekani

MSIMU huu wa Kombe la Dunia unaelekea ukingoni. Fainali itachezwa kesho Jumapili, Julai 19, 2026, katika Uwanja wa MetLife nchini Marekani, ikizikutanisha Argentina na Hispania.

Kwa mwezi mmoja wa michuano hiyo iliyoanza Juni 11, 2026, zimeshuhudiwa mechi kali na zilizoacha msisimko mkubwa kwa wapenzi wa soka duniani.

PARAGUAY 1-1 UJERUMANI

Mechi ya hatua ya 32 Bora, ambayo ilichezwa Juni 29 na kumalizika kwa sare ya bao 1-1, kabla ya Paraguay kuitoa Ujerumani kwa mikwaju ya penalti (4-3).

Paraguay iliwashangaza wengi kwa ushindi huo kwani Ujerumani ndiyo iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kusonga mbele.

MOROCCO 1-1 UHOLANZI

Mechi ya hatua ya 32 iliyochezwa Juni 29, ambayo dakika zake 120 za uwanjani zilimalizika kwa sare ya bao 1-1, kabla ya Morocco kushinda kwa penalti 3-2.

Katika mchezo huo, Uholanzi walioonekana wameshamaliza kazi baada ya Cody Gakpo kuifungia bao dakika ya 72, lakini Issa Diop alizawazisha sekunde chache baada ya zile 90 kumalizika.

HISPANIA 2-0 UFARANSA

Ni nusu fainali iliyochezwa Julai 14. Licha ya uwepo wa Kylian Mbappe, Ousmane Dembele, Michael Olise na Bradley Barcola, iliwachukua dakika 82 kupata shuti la kwanza lililolenga lango.

Miaka miwili iliyopita, 2024, Hispania iliifunga Ufaransa katika hatua kama hii kwenye michuano ya EURO. Ni kama ilivyokuwa mwaka huu (2026) katika nusu fainali ya Nations League.

CAPE VERDE 0-0 HISPANIA

Ilikuwa mechi ya hatua ya makundi na ilichezwa Juni 15. Cape Verde wakishikiriki kwa mara ya kwanza, walishangaza dunia kwa kuambulia suluhu mbele ya vigogo Hispania.

Katika mchezo huo, Cape Verde walionesha uvumilivu mkubwa kwani licha ya Hispania kupiga mashuti 27, ni saba pekee yaliyolenga lango, ambayo pia hayakuzaa bao.

UBELGIJI 3-2 SENEGAL

Mechi ya hatua ya 32 Bora na ilichezwa Julai Mosi. Senegal walikuwa mbele kwa mabao 2-0 hadi dakika ya 86, kabla ya Romelu Lukaku na Youri Tielemans kuisawazishia Ubelgiji.

Katika dakika ya 125, Ubelgiji ilipata penalti kupitia VAR na Tielemans akapiga na kufunga.

ARGENTINA 2-1 ENGLAND

Nusu fainali iliyochezwa Julai 15. Baada ya England kupata bao la kuongoza, kocha Thomas Tuchel alichagua kujilinda na wakati fulani akitumia mabeki sita uwanjani.

Lilikuwa kosa kubwa. Enzo Fernandez aliizawazisha Argentina katika dakika ya 85, kabla ya Lautaro Martinez naye kufunga bao la ushindi. Asisti zote zilitoka kwa nahodha Lionel Messi.

URENO 2-1 CROATIA

Hiyo ilikuwa mechi ya hatua ya 32 Bora na ilichezwa Julai 2. Ureno ya Cristiano Ronaldo (41) dhidi ya Croatia ya Luka Modric (40).

Ureno wakiwa mbele kwa mabao 2-1, Croatia walipata bao dakika za mwisho kupitia kwa beki Josko Gvardiol lakini VAR ilibaini kuwa Mario Pasalic alikuwa kwenye eneo la kupotea wakati anatoa ‘asisti’.

ARGENTINA 3-2 MISRI

Hiyo ni mechi ya hatua ya 16 Bora iliyochezwa Julai 7. Misri waliweza kuongoza kwa mabao 2-0 hadi Christian Romero alipofunga dakika ya 79, kisha Lionel Messi kuongeza jingine dakika nne tu baadaye.

Katika dakika za mwisho, bao la kichwa la Enzo Fernandez lilizima kabisa matumaini ya Misri, ingawa nayo ilifunga bao lililokataliwa na VAR na kuzua mjadala mkubwa.

ENGLAND 3-2 MEXICO

Timu hizo zilikutana Julai 5 kwa mchezo wa hatua ya 16 Bora. Mexico watamkumbuka Jude Bellingham kwa mabao yake mawili ndani ya dakika tatu, kabla ya Julian Quinones kuwapa bao moja muda mfupi kabla ya mapumziko.

Hata hivyo, England waliongeza la tatu kupitia penalti ya Harry Kane, kabla ya Raul Jimenez kuipatia Mexico bao la kufutia machozi dakika ya 69.

ARGENTINA 3-2 CAPE VERDE

Mechi ya hatua ya 32 Bora. Ilichezwa Julai. Ni mchezo ambao Argentina waliongoza mara mbili tofauti lakini Cape Verde waliweza kusawazisha.

Kwa sare ya mabao 2-2, mchezo ulilazimika kuhamia dakika 120, kabla ya Argentina kupata bao la ushindi dakika ya 111.

Related articles

Recent articles