30.3 C
New York

Davido afichua kuhusu watoto wake

Published:

LAGOS, Nigeria 

STAA wa Afrobeats, David Adeleke, maarufu Davido, amesema watoto wake wamemuuliza kwanini hawakupatikana kwa mama mmoja.

Mwanamuziki huyo ana watoto sita katika mahusiano yake na wanawake tofauti. Ana mabinti mapacha katika ndoa yake ya sasa na Chioma Adeleke.

Katika mahojiano yake na BBC, Davido amesema watoto wanaomuuliza juu ya kutokuwa na mama mmoja ni mabinti zake wakubwa, Imade na Hailey.

“Watoto wangu wamefikia umri ambao sasa wanawauliza sababu ya kuwa na mama tofauti na kwanini siishi nao,” amesema.

Ukiacha Chioma anayeishi naye, wanawake wengine waliowahi kumpatia watoto ni Sophia Momodu na Larissa Yasmin Lorenco.

Related articles

Recent articles