MIAMI, Marekani
LICHA ya kucheza mechi zaidi ya 200 akiwa na timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi hajawahi kuikabili England.
Safari hii, Messi atakutana kwa mara ya kwanza na ‘Three Lions’ katika mchezo wa nusu fainali ya msimu huu wa Kombe la Dunia.
Argentina ya Messi imeingia nusu fainali baada ya ushindi wake wa mabao 3-1 dhidi ya Mexico, mchezo uliofika dakika 120.
Katika mechi hiyo, Messi kwa mara ya kwanza msimu huu wa Kombe la Dunia aliondoka uwanjani bila kuziona nyavu.
Kuelekea nusu fainali hiyo, mkongwe wa England, Wayne Rooney, amewaonya wachezaji wa timu hiyo akisema inahitaji umakini mkubwa kumzuia Messi asilete madhara.
“Kumdhibiti Lionel Messi ni kutuliza akili na kuwasiliana. Kuwasiliana na wenzako wakati wote ili wakae eneo ambalo umehama,” amesema.


