27.2 C
New York

Kiti cha Nabi hakikaliki Yanga?

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

TANGU Nasreddine Nabi alipoondoka mwaka 2023, kibarua cha benchi la ufundi la Yanga kimekuwa kigumu kwa kila kocha aliyeingia klabuni hapo.

Kwa ufupi, makocha sita wameingia na kutoka Jangwani tangu Nabi alipoiachia Yanga mafanikio makubwa ya kufika fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Nabi raia wa Tunisia, alipoondoka Mei, 2023, baada ya misimu miwili ya kufanya kazi, Cedric Kaze wa Burundi ndiye aliyekalia benchi la ufundi kwa muda.

Alipoondoka Kaze, aliajiriwa Miguel Gamondi, ambaye alianza kazi Julai, 2023, kisha naye akafungasha virago vyake mwaka 2025.

Kutimka kwa Gamondi kulimfungulia mlango Saed Ramovic kutua Jangwani lakini naye hakuumaliza mwaka 2025, akaondoka na kumpisha Abdi Hamid Moalin.

Moalin alishika kwa muda mfupi pia, kabla ya uongozi wa Yanga kumtangaza raia wa Ufaransa, Roman Folz, kuwa kocha wake mpya.

Tofauti na matarajio ya wengi, Folz hakudumu Jangwani, na badala yake aliiacha mikoba kwa kocha raia wa Ureno, Pedro Goncalves.

Kama ilivyotokea kwa wenzake, Goncalves hakuweza kubaki Yanga kwa muda mrefu, hivyo kuondoka na klabu hiyo kumrudisha Moalin kwa muda.

Moalin, licha ya kuiongoza Yanga kumaliza msimu wa 2025-26 ikiwa bingwa wa Ligi Kuu Bara, bado naye ametimka.

Na sasa, benchi la ufundi la vigogo hao wa Kariakoo liko kwenye mikono ya kocha mpya, Manqoba Mngqithi.

Kocha huyo raia wa Afrika Kusini amewahi kuzinoa kwa nyakati tofauti klabu za Mamelodi Sundowns, Amazulu, Chippa United na Golden Arrows.

Je, ataepuka mkosi uliowakuta wenzake waliojaribu kuziba pengo la Nabi au naye kitamkuta? Ni suala la muda.

Related articles

Recent articles