27.2 C
New York

Bellingham aandika historia akiichapa Norway

Published:

LONDON, Uingereza

KIUNGO wa kimataifa wa England, Jude Bellingham, ameweka rekodi baada ya mabao yake mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Norway katika robo fainali ya Kombe la Dunia.

Mchezo huo ulichezwa jana Julai 11, 2026 na England kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.

Bellingham amekuwa mchezaji wa saba wa England kufunga mabao mawili katika mechi mbili mfululizo za hatua ya matoano katika historia ya Kombe la Dunia.

Kabla ya kuiadabisha Norway, kiungo huyo alipasia nyavu mara mbili katika mchezo uliopita wa hatua ya 16 Bora dhidi ya Mexico.

Kwa matokeo hayo, England sasa wanaisubiri Argentina ya mkali Lionel Messi katika hatua ya nusu fainali.

Related articles

Recent articles