Na mwandishi wetu, Gazetini
TANZANIA imebaki katika nafasi yake ya 112 kwenye viwango vipya vya ubora wa soka duniani vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Ni kama ilivyo kwa majirani zake wa Afrika Mashariki, Uganda na Kenya, ambazo pia zimebaki pale pale katika nafasi ya 89 na 109 duniani.
Kwa mujibu wa ripoti ya viwango vipya hivyo, Tanzania imebaki nafasi yake ya 112 ikiwa imekusanya pointi 1180.78.
Wakati huo huo, Ufaransa imepanda kwa nafasi mbili na kushika namba moja kwenye viwango hivyo, ikifuatiwa na Hispania, Argentina, England na Brazil.
Kwa upande mwingine, Morocco ndiyo imepanda kwa nafasi moja na sasa inashika nafasi ya kwanza kwa ubora barani Afrika.


