21.8 C
New York

Waasi washambulia kambi ya jeshi

Published:

BAMAKO, Mali

KIKUNDI cha waasi nchini Mali kimeishambulia kambi ya jeshi, pamoja na gereza, katika maeneo ya Kaskazini, Kati na Kusini, jirani na Mji Mkuu wa Bamako.

Shambulizi hilo limefanywa na Kundi la FLA la mjini Tuareg, ambalo limekuwa likishinikiza uhuru wa Jimbo la Azawad ili kuongozwa kwa sheria za Dini ya Uislam (Sharia).

Aidha, shambulizi hilo, pamoja na lile la Aprili, 2026, ni mwendelezo wa hali mbaya ya usalama inayoikumba Mali chini ya utawala wa kijeshi.

Itakumbukwa, jeshi lilipindua Serikali mwaka 2020 lakini ahadi yake ya kurejesha amani haijazaa matunda.

Kuhusu shambulizi jipya, jeshi limesema waasi wamelenga Mji wa Gao, ambao ndiyo mkubwa zaidi Kaskazini-Mashariki mwa Mali.

Wakazi wa Gao wamekiri kusikia milio ya risasi na ndege za kivita jirani na kambi hiyo, kwa mujibu wa taarifa.

Related articles

Recent articles