TORONTO, Canada
TIMU 13 zimeshakata tiketi ya kucheza hatua inayofuata ya 16 Bora msimu huu wa fainali za Kombe la Dunia.
Ni baada ya Uswis nayo kuvuka 32 Bora kwa ushindi wa mabao 2-0 walioupata dhidi ya wawakilishi wa Afrika, Algeria.
Katika mchezo huo, Uswis walipata mabao yao kupitia kwa Dan Ndoye na Breel Embolo.
Kwa matokeo hayo, Uswis wataivaa Colombia katika mchezo mgumu wa hatua ya 16 Bora.
Aidha, timu zingine zilizoingia hatua hiyo ni Ubelgiji, Ufaransa, Brazil, Norway, Morocco, Paraguay, Canada, Mexico, England, Ureno, Hispania na Marekani.


