TORONTO, Canada
MKONGWE wa soka la Liberia, George Weah, ambaye ni Mwafrika pekee kuwahi kubeba Ballon d’Or, amesema Kylian Mbappe ni bora kuliko Lamine Yamal.
Weah aliyewahi pia kuwa Raia wa Liberia, amesema Yamal raia wa Hispania bado anakua, hivyo bado hajafikia ukomavu wa Mbappe.
“Lamine Yamal bado anakua. Naamini ataendelea kuwa bora. Lakini usimfananishe na Mbappe. Hakuna asiyejua kwamba Mbappe yuko mbali sana,” ameasema straika huyo wa zamani wa AC Milan.
Kauli ya Weah inakuja wakati huu Mbappe akiwa moto wa kuotea mbali msimu huu wa Kombe la Dunia.
Nyota huyo wa timu ya soka ya Taifa ya Ufaransa ameshaingia kambani mara sita, wakati Yamal wa Hispania ana bao moja pekee.


