27.8 C
New York

Trump alivyokwama kufuta uraia wa kuzaliwa

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

MAHAKAMA Kuu ya Marekani imezuia jaribio la Rais Donald Trump aliyetaka kufuta uraia wa kuzaliwa, ambao umekuwa ukitambulika katika sheria za nchi hiyo tangu mwaka 1868.

Ikimanisha kwamba kuzaliwa Marekani kunakupa haki ya kuwa raia wa Taifa hilo, bila kujali uraia wa wazazi wako.

Taasisi ya Sera ya Uhamizaji nchini Marekani inakadiria kuwa watoto 255,000 huzaliwa na kupata uraia wa Marekani kila mwaka kwa kuzaliwa na wazazi ambao si raia wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Trump na Makamu wake wa Rais, JD Vance, hiyo ni sera mbovu na imekuwa chanzo cha wahamiaji haramu nchini kwao.

Hata hivyo, kuna idadi kubwa ya wanasiasa maarufu na wengine ni watu wa karibu wa Trump waliopata uraia wa Marekani kwa kuzaliwa.

Miongoni mwao ni Katibu Mkuu wa Serikali, Marco Rubio, Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (FBI), Kash Patel, na hata mke wa Vance, Usha Vance.

Kwa upande mwingine, licha ya Rais Trump kudai kuwa Marekani ndiyo nchi pekee inayompa uraia kila mtoto anayezaliwa, bila kujali wanakotoka wazazi wake, tafiti zinaonesha tofauti.

Mathalan, utafiti wa Kituo cha Tafiti cha Pew umeainisha nchi 32 duniani, ambazo nazo zina utaratibu huo wa kumpa uraia mtoto anayezaliwa.

Miongoni mwazo ni baadhi ya nchi za Amerika ya Kaskazini na Latin ya Amerika.

Ni tofauti na Ugiriki, Iran, Ufaransa na Morocco, ambako mtoto atapewa uraia endapo tu wazazi wake walizaliwa katika nchi hiyo.

Kwa nchi za Australia, Ujerumani na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), mtoto atapewa uraia hata ikiwa wazazi wake ni wahamiaji wanaoishi kihalali. Siyo walioingia kwa ‘njia za panya’.

Related articles

Recent articles