37.6 C
New York

Mshambuliaji anayesakwa na vigogo EPL

Published:

LONDON, Uingereza

NI nahodha wa West Ham United, Jarrod Bowen, ambaye si tu Manchester United, bali pia Liverpool na Chelsea nazo zinaimezea mate saini yake.

Mshambuliaji huyo ni mchezaji mwingine muhimu anayejiandaa kuondoka West Ham baada ya klabu hiyo kumuuza Mateus Fernandes aliyetua Tottenham kwa Pauni milioni 85.

Nyota wengine walio njiani kutimka klabuni hapo ni Crysencio Summerville, Aaron Wan‑Bissaka na Jean-Clair Todibo.

Bowen ameingia kwenye rada za klabu kubwa za Ligi Kuu ya England (EPL), licha ya kwamba amebakiza miaka minne katika mkataba wake na West Ham.

Msimu wa 2025-26 ulikuwa mzuri kwa Muingereza huyo, ambapo aliumaliza akiwa na mabao 11 na ‘asisti’ 11 katika mechi 38 za EPL.

Kwa takwimu za jumla, nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 ameshacheza mechi 280 akiwa na ‘uzi’ wa West Ham, akifunga mabao 85 na asisti 63.

Related articles

Recent articles