TEHRAN, Iran
MAKAO Makuu ya Jeshi la Iran yamekuja na tamko zito, kwamba Marekani itaingia kwenye shida endapo itaendelea kuingilia udhibiti wa Mlango-Bahari wa Hormuz.
Kauli hiyo inakuja wakati huu uhusiano wa mataifa hayo ukiwa umezorota mara dufu, licha ya mazungumzo ya awali ya kumaliza vita.
Hata hivyo, mamlaka za Iran zimeendelea kusisitiza kuwa Taifa hilo la Kiarabu ndilo linaloshikili udhibiti wa Hormuz.
Hormuz ni njia ya maji muhimu kwa uchumi, ikitumika kufikisha kwenye soko la dunia asilimia 20 ya mafuta na gesi.
Awali, Iran iliufunga Mlango-Bahari huo, hatua iliyosababisha uhaba na kupanda wa bei ya mafuta duniani.
Hivi karibuni, Marekani na Iran zilifikia makubaliano ya kumaliza vita ndani ya siku 60. Vita kati ya nchi hizo vilianza Februari 28, 2026.
Hata hivyo, siku chache tu baada ya makubaliano hayo, pande mbili hizo zilianza kushambuliana, hali inayoendelea hadi sasa.


