31.1 C
New York

TRA, JKT wana vita yao wenyewe Ligi Kuu Bara

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini

KAMA ilivyokuwa msimu uliopita (2024-25), safari hii TRA United na JKT zimerudi kwenye ‘bato’ yao ya Ligi Kuu Bara.

Msimu uliopita, TRA ilimaliza katika nafasi ya tano ikiwa na pointi 38, huku JKT wakiwa nyuma yao kwa tofauti ya pointi mbili.

Safari hii, huku kila timu ikiwa imebakiza mechi moja kuelekea mwisho wa msimu Juni 30, 2026, msimamo uko hivyo hivyo, tofauti ikiwa ni idadi ya pointi tu.

TRA ya Tabora iko nafasi ya tano ikiwa na pointi 42, sawa na JKT iliyo chini yake, zikitofautina mabao ya kufunga na kufungwa tu.

Je, TRA inaendelea kushika nafasi ya tano kama ilivyokuwa msimu uliopita au ni zamu ya JKT kukaa juu yao?

Hata hivyo, hakuna itakayoweza kufikia Singida Black Stars inayohitimisha ‘Top 4’ kwani tayari timu hiyo ina pointi 50 ikiwa na mechi moja mkononi.

Related articles

Recent articles