24.3 C
New York

Yanga yaifumua TRA, Okello ana balaa zito

Published:

Na Hassan Mwasha

KATIKA mwendelezo wa kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara, Yanga imeibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya TRA United.

TRA, licha ya kupewa nafasi kubwa ya kuisumbua Yanga, imeungana na Azam, ambayo siku chache zilizopita iligongwa na Yanga kwa kichapo kama hicho katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Katika mchezo wa leo Juni 27, 2026, uliochezwa katika Uwanja wa KMC, Mwenge jijini Dar es Salaam, mabao yote ya Yanga yalipachikwa na mshambuliaji raia wa Uganda, Allan Okello.

Mshambuliaji huyo alifunga bao la kwanza katika dakika 27, akaweka la pili dakika ya 51 (penalti), kabla ya kufunga kitabu dakika ya 60.

Kwa upande mwingine, hiyo inakuwa ‘hat-trick’ ya kwanza kwa nyota huyo tangu alipojiunga na Yanga wakati wa usajili wa dirisha dogo msimu huu wa 2025-26.

Hivyo, sasa Okello anafikisha mabao 14 tangu alipoingia Ligi Kuu Bara akitokea Vipers ya Uganda.

Related articles

Recent articles