24.3 C
New York

Marekani, Iran ‘kimenuka’ tena

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

JESHI la Marekani limeishambulia Iran, zikiwa ni saa chache tu tangu Rais Donald Trump aliposema wenzao hao wamekiuka makubaliano ya Juni 17, 2026.

Katika taarifa yake, Rais Trump amesema wamejibu mapigo baada ya Iran kushambulia meli yake ya mizigo iliyokatiza Mlango-Bahari wa Hormuz.

Kwa upande wake, Iran imekiri kutekeleza shambulizi hilo kwa kutumia ndege zisizo na rubani, ikidai kuwa Marekani ilikiuka taratibu za kupita katika eneo hilo.

Kujibu shambulizi hilo, vikosi vya jeshi la Marekani jana Juni 26, 2026, vilishambulia maeneo nyeti ya Iran, vikiwamo vituo vyake vya ndege zisizo na rubani.

Lakini, mamlaka za Iran zinaitaja Marekani kuwa ya kwanza kukiuka makubaliano ya matumizi ya Hormuz.

“Kama hali itaendelea kuwa hivi, basi majibu yetu nayo yatakuwa hivyo au zaidi ya hapo,” imeeleza taarifa ya Jeshi la Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC).

Aidha, mtifuano huo unakuja wakati tayari Marekani na Iran zilikubaliana kusitisha vita hivyo vilivyoanza tangu Februari 28, 2026.

Related articles

Recent articles