Na CHRISTOPHER MSEKENA
JANGA la ugonjwa wa Ebola limeendelea kuwa tishio nchini Kongo baada ya ndugu wa watano wa mwimbaji wa Injili Jonathan Budju, kupoteza maisha mapema mwezi huu.
Jonathan Budju ambaye kwasasa anaishi nchini Canada, ameweka wazi kuwa binamu yake mchungaji Enock Bahwere mama yake, dada kaka na shemeji yake kwenye janga hilo la Ebola linalotikisa mji wa Ituli, Bunia.

Akizungumza na gazetini.com Jonathan amesema huo ni msiba mkubwa kwake na kwa familia yake hiyo inayoishi Mashariki wa Kongo na jamii inapaswa kuchukua tahadhali.
“Nimepoteza ndugu zangu wa karibu, shangazi yangu amefariki lakini pia binamu na shemeji zangu nao wamefariki kwa Ebola, hali inatisha na jamii inapaswq kuendeleza kampeni ya kupinga ugonjwa huu hatari huko nyumbani Kongo,” amesema Jonathan.



