27.9 C
New York

The Living Testimony ya Bernard Mwambungu yazidi kupaa

Published:

Na Christopher Msekena

MWIMBAJI wa muziki wa Injili nchini, Bernard Mwambungu, amewashukuru mashabiki kwa mapokezi makubwa ya albamu yake The Living Testimony.

Mwambungu ameanza kuachia nyimbo kadhaa kutoka kwenye albamu hiyo kama vile Mungu Mkuu, Ushuhuda, Story ya Mtu Mmoja, Wewe ni Baba na Ni Mzuri Wewe.

Akizungumza na gazetini.com, Bernard Mwambungu amesema ndani ya muda mfupi tangu kuachiwa kwa nyimbo hizo mfululizo, imefanikiwa kupata wasikilizaji na watazamaji wengi tofauti na matarajio yake.

“Albamu ya Ushuhuda Unaoishi au The Living Testimony imenifungulia njia zaidi hu hapa nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Nimepata idadi kubwa ya watazamaji kwenye chaneli yangu ya YouTube, naamini wanaendelea kunipa sapoti ili nizidi kutangaza injili,” amesema Mwambungu.

Related articles

Recent articles