MUNICH, Ujerumani
LEJENDARI wa Bayern Munich, Thomas Muller, ameishauri klabu ya Manchester United kumsajili kiungo wa Freiburg, Johan Manzambi.
Ushauri wa Muller umetokana na kiwango kizuri alichokionesha nyota huyo wa timu ya soka ya Taifa ya Ujerumani katika fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea.
Manzambi ndiye aliyefunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 walioupata Ujerumani mbele ya Bosnia.
Man United na klabu zingine kubwa za Ulaya ziko kwenye mbio za kumfukuzia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20.
“Ni mchezaji mzuri kwa ujumla. Amekuwa kwenye macho yetu kwa muda mrefu sasa,” amesema Muller na kuitaka Bayern Munich nayo kumzingatia Manzambi.


