MADRID, Hispania
BEGONA Gomez ambaye ni mke wa Waziri Mkuu wa Hispania, Pedro Sanchez, amewekewa zuio la kusafiri nje ya nchi wakati huu akikabiliwa na mashitaka ya kujihusisha na rushwa.
Mahakama imetoa taarifa hiyo leo Juni 20, 2026, ikimtaka pia kukabidhi hati yake ya kusafiria.
Sambamba na hilo, Begona amepewa utaratibu wa kufika mahakamani mara mbili kila mwezi.
Kwa mujibu wa taarifa, biashara zake zinahusishwa na rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma.
Kwa upande wake, Begona anasisitiza kuwa hauhusiki katika yote hayo anayohusishwa nayo.


