17.4 C
New York

Hawa hapa mastaa wapya Arsenal

Published:

LONDON, Uingereza

MAPEMA tu! Kwa taarifa yako, Arsenal wameashaanza mipango ya kuutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) msimu ujao (2026-27).

Wakati huu fainali za Kombe la Dunia zikiendelea, kocha Mikel Arteta na Mkurugenzi wa Michezo klabuni hapo, Andrea Berta, wanasuka mipango ya usajili wa kiangazi.

Wawili hao walitumia Pauni milioni 250 sokoni msimu wa 2025-26 na matokeo yake wakabeba ‘ndoo’ ya EPL, pamoja na kufika hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Winga wa kushoto wa Club Brugge ya Ubelgiji, Christos Tzolis, ameingia kwenye rada zao na huenda Arsenal ikatumia Pauni milioni 35 kumnasa.

Pia, Arteta anataka safu yake ya kiungo iimarishwe zaidi na sasa Arsenal inamfuatilia kiungo wa Lille aliyeko Kombe la Dunia akiwa na Morocco, Ayyoub Bouaddi.

Ripoti zinaeleza kuwa Lille ya Ufaransa haina shida, ingawa inataka iwekewe mezani kitita cha Pauni milioni 60 ili kumfungulia mlango wa kutokea.

Related articles

Recent articles