34.1 C
New York

Shabiki afariki akiingia uwanjani Kombe la Dunia

Published:

MEXICO CITY, Mexico

SHABIKI wa soka mwenye umri wa miaka 80 amefariki muda mfupi kabla ya kuingia uwanjani kuitazama Mexico ikivaana na Afrika Kusini katika mchezo wa ufunguzi wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu.

Taarifa zinaeleza kuwa shabiki huyo alipata shambulio la moyo akiwa geti namba moja la Uwanja wa Azteca.

Wahudumu wa afya wa dharura uwanjani hapo walimkimbilia na kumpatia huduma ya kwanza, kabla ya kumkimbiza hospitali akiwa kwenye hali nzuri.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa rasmi ya mamlaka za Mexico, shabiki huyo ambaye jina halikufahamika mara moja, alifariki akiwa anaendelea na matibabu.

Mechi hiyo ya Kundi A ilianza baada ya shoo kali ya jukwaani kutoka kwa wanamuziki mbalimbali, wakiwamo Shakira na Burna Boy, walioimba pamoja wimbo wao maalumu wa fainali za mwaka huu uitwao ‘Dai Dai’.

Related articles

Recent articles