25.9 C
New York

Zelensky amuomba Putin wayamalize

Published:

KYIV, Ukraine

RAIS wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amemuomba mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin, wakutane na kuzungumza juu ya kumaliza vita vinavyoendelea kati ya mataifa mawili hayo.

Katika barua yake kwa Putin, Zelensky amemtaka mwenzake huyo kukubali kukaa mezani ili kumaliza vita, kabla ya Marekani kuingilia.

Katika barua hiyo, amesema namna pekee ya Urusi na Ukraine kurejesha utulivu ni yeye na Putin kukutana na kutafuta suluhisho.

Wito huo wa Zelensky unakuja zikiwa ni siku chache tu zimepita tangu Putin alipoweka wazi kuwa hana mpango wa kuitisha mapigano na Ukraine.

Wakati huo huo, Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema litakuwa jambo na lenye afya kwa viongozi hao kukutana kwa masilahi ya Ukraine na Urusi.

Related articles

Recent articles