30 C
New York

Waandamanaji Libya wavamia, wafanya fujo ofisi za UN

Published:

TRIPOLI, Libya

WANANCHI wa Libya walioingia barabarani kupinga taarifa za nchi yao kupokea wahamiaji kutoka Marekani wameingia na kufanya vurugu katika ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo Magharibi mwa Mji Mkuu wa Tripoli.

Katika video zilizopo kwenye mitandao ya kijamii, waandamanaji wanaonekana wakizuia shughuli zote katika ofisi ya Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) wilayani Sarraj.

Katika ujumbe wao, wameitaka ofisi ya UNHCR kuondoka nchini Libya na kuacha mara moja mpango wa kupeleka wahamiaji wanaotoka Marekani.

Hata hivyo, Serikali ya Libya imeeleza kushangazwa na taarifa hiyo, ikieleza kuwa ilishakataa ombi la kupokea wahamiaji hao.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Libya, nchi hiyo inashikilia msimamo wake wa kutokubaliana na programu hiyo.

Related articles

Recent articles