30 C
New York

Hezbollah yasema haiko tayari kusitisha vita

Published:

NABATIEH, Lebanon

Pande mbili hizo zimeingia kwenye mapigano ya muda mrefu sasa, hasa tangu Hezbollah ilipoamua kuisaidia Iran ilipoanza kushambuliwa na Marekani na Israel mwanzoni mwa mwaka huu (Februari 28, 2026).

Kwa upande wa Hezbollah, wamesema wanachohitaji ni kuona vikosi vya jeshi la Israel vikiondoka Kusini mwa Lebanon na si vinginevyo.

Wakati huo huo, Serikali ya Israel chini ya Waziri Mkuu wake, Benjamin Netanyahu, ameendelea kusisitiza kuwa haina mpango wa kuondoka katika maeneo hayo ya mpaka wake na Lebanon.

Kwa mujibu wa Israel, kukaa kwao Kusini kwa Lebanon ni katika kujilinda dhidi ya Hezbollah inayotumia maeneo hayo kuishambulia.

Related articles

Recent articles