30 C
New York

Ajali ya moto hotelini yaua watu 21

Published:

NEW DELHI, India

RAIA wa kigeni 21, wakiwamo wa Nigeria, Msumbiji na Liberia, wamepoteza maisha katika ajali ya moto iliyotokea katika hoteli moja mjini Delhi.

Wizara ya Mambo ya Nje ya India imethibitisha kutokea kwa ajali hiyo Juni 3, 2026, ikieleza kuwa polis wanaendelea kuchunguza chanzo chake.

“Wizara ya Mambo ya Nje ya India inaendelea kuwasiliana na balozi za nchi husika, pamoja na kutoa msaada kwa kadiri inavyowezekana,” amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Subrahmanyam Jaishankar.

Katika hatua nyingine, polisi wameripotiwa kumshikilia mmiliki wa hoteli hiyo, Lavkesh Bajaj, aliyekamatwa saa chache baada ya jengo hilo kuwaka moto.

Hata hivyo, majanga ya moto katika hoteli nchini India imekuwa ni kawaida, ikikumbukwa kuwa lipo tukio kubwa zaidi la mwaka 2022 mjini Delhi.

Related articles

Recent articles