26 C
New York

Saba wafariki baada ya ‘drone’ kugonga basi la abiria

Published:

KYIV, Ukraine

WATU saba wameripotiwa kupoteza maisha na wengine 11 kujeruhiwa baada ya ndege isiyo na rubani (drone) kugonga basi la abiria nchini Ukraine.

Kwa mujibu wa kiongozi wa Mkoa wa Donetsk, Mashariki mwa Ukraine, ajali hiyo imetokea leo Juni 3, 2026 katika eneo la Crimea linalodhibitiwa na Urusi.

Aidha, ajali hiyo imekuja wakati Urusi ikiwa imetekeleza mashambulizi kadhaa ya ndege zisizo na rubani katika maeneo mengi ya Ukraine.

Katika mashambulizi hayo, imeripotiwa kuwa watu takribani 22 wamepoteza maisha, huku wengi wakiwa ni wanawake na watoto.

Vita kati ya nchi hizo vimeendelea kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu katika nchi zote mbili tangu Urusi ilipochukua hatua ya kuivamia Ukraine.

Related articles

Recent articles