LAGOS, Nigeria
MWANAMUZIKI wa Afrobeats, Divine Ikubor, maarufu kwa jina la Rema, amesema mpenzi wake alikuwa mkorofi na msumbufu, hivyo akaamua kuachana naye na kubaki ‘singo’.
Katika mahojiano yake na staa wa YouTube, Korty EO, Rema amesema uhusiano ulikuwa mzuri lakini haukuwa na amani.
Amesema wakati mwingine alirudi nyumbani aliamini angekwenda kupumzika lakini aliishia kukutana na ugomvi tu.
“Unaporudi nyumbani, unategemea kwenda kutulia. Unapokutana na presha zingine, unakuwa kwenye wakati mgumu zaidi,” alisema.
Kwa upande mwingine, alipoulizwa kama ana mpango wa kurudi kwenye mahusiano kwa siku za hivi karibuni, Rema alijibu hapana.


