ANKARA, Uturuki
MAELFU ya wananchi wa Uturuki wameingia barabarani kupinga uamuzi wa Mahakama kutokumtambua kiongozi wa upinzani, Ozgur Ozel.
Ozel ameondoshwa katika nafasi yake ya uongozi wa juu ndani ya Chama Kikuu cha upinzani cha Republican People’s Party (CHP).
Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama mjini Ankara kusema Mkutano uliomchagua Mei 21, 2026 kuwa Mwenyekiti ulikuwa batili na ushindi wake ulitokana na kukiukwa kwa baadhi ya taratibu.
Hata hivyo, uamuzi wa Mahakama umehusishwa na mpango wa kudhohofisha upinzani kwa kumzuia Ozel kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais wa nchi hiyo.
Kwamba mamlaka zinamuona mwanasiasa huyo kama tatizo kwa Rais Recep Tayyip Erdogan katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2028.


