20.9 C
New York

Kesi ya Duterte kuanza kusikilizwa Novemba 30

Published:

NEW YORK, Marekani
MAHAKAMA ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) imetangaza Novemba 30, 2026, kuwa ndiyo siku ya kuanza kusikilizwa kwa kesi ya Rais wa zamani wa Ufilipino, Rodrigo Duterte.
Aliiongoza Ufilipino kuanzia mwaka 2016 hadi 2022 na kwa sasa anakabiliwa na mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Duterte (81), anatajwa kusababisha mauaji na udhalilishaji wa kingono kwa maelfu ya watu wakati wa operesheni yake ya kudhibiti dawa za kulevya nchini humo.
Kwa mujibu wa ICC, alifanya ukatili huo kuanzia Novemba Mosi, 2011, hadi Machi 16, 2019, ikiwamo wakati akiwa Meya wa Jimbo la Davao, Kusini mwa Ufilipino.
Mwanasiasa huyo amekuwa akishikiliwa na ICC mjini The Hague, Uswis, tangu alipokamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Manila mwanzoni mwa mwaka 2025. Anakuwa kiongozi wa kwanza wa Asia kufikishwa mbele ya Mahakama hiyo.

Related articles

Recent articles