25 C
New York

Mshindi Big Brother ajuta kuwasaidia ndugu

Published:

LAGOS, Nigeria

MSHINDI wa Msimu wa 7 wa Shindano la Big Brother Naija, Josephina Ijeoma Otabor ‘Phyna’, ameeleza kujutia uamuzi wake wa kutumia fedha alizopata kuwasaidia ndugu, badala ya kuwekeza.

Itakumbukwa kuwa Phyna ni mshindi wa mwaka 2022, ambapo aliondoka na kitita cha Naira milioni 100.

Akihojiwa hivi karibuni, amesema si tu alikuwa na umri mdogo, bali pia alikuwa na ‘ushamba’ wa kumiliki fedha nyingi, hivyo kujikuta akishindwa kuwekeza kwenye biashara.

Katika hatua nyingine, amesema anawalamu zaidi ndugu zake, ambapo waliishia kumuomba msaada wa kifedha badala ya kumpa ushauri wa kifedha.

Ameongeza kuwa ndugu hao walimgeuka na kumwacha peke yake walipoona ameishiwa. “Kwa sasa, fedha zimeisha, nimebaki napambana na hali yangu,” amesema Phyna.

Related articles

Recent articles