25 C
New York

Israel yatangaza kumuua kamanda wa Hamas

Published:

JERUSALEM, Palestina

JESHI la Israel limetangaza kufanya shambulizi katika Ukanda wa Gaza na kumuua kiongozi wa wapiganaji wa Kundi linalohusishwa na ugaidi la Hamas.

Taarifa ya Israel imeeleza kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa jana Mei 26, 2026 na kuondosha uhai wa kamanda Mohammed Odeh.

Kwa mujibu wa mashuhuda, raia watatu wa Palestina wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa katika shambulizi hilo lililolenga eneo la soko.

Wakati huo huo, Israel wamedai kuwa baada ya upelelezi wa miezi mingi, walibaini makazi aliyokuwa amejificha kamanda Odeh na kuyashambulia.

Hata hivyo, bado uongozi wa Hamas haujazungumza chochote kuthibitisha au kukanusha juu ya taarifa za kuuawa kwa kiongozi wao.

Israel na Hamas wameendelea kushambuliana, licha ya makubaliano ya Oktoba, 2025, ambapo pande mbili hizo ziliafiki kusitisha mapigano ili kuruhusu mazungumzo ya kutafuta suluhu.

Related articles

Recent articles