18 C
New York

Xavi, Chelsea kumbe tetesi tu

Published:

CATALUNYA, Hispania

LICHA ya tetesi zilizopo, Chelsea hawana mpango wa kumpa ajira kocha wa zamani wa Barcelona raia wa Hispania, Xavi Hernandez.

Awali, zilikuwepo taarifa zilizodai kuwa Blues wamewasiliana na wakala wake ili akazibe pengo la Liam Rosenior aliyefukuzwa hivi karibuni.

Chelsea wamekuwa chini ya makocha wa kudumu wanne kwa kipindi kifupi cha miaka minne ya uongozi wa mabosi wapya, BlueCo.

Rosenior aliziba pengo la Enzo Maresca lakini Muingereza huyo amefukuzwa baada ya siku 106 tu tangu alipoajiriwa.

Xavi (46), amekuwa nje ya kazi tangu alipoondoka Barcelona mwaka 2024, akikumbukwa kwa taji moja la La Liga na kuibua vipaji vya Pau Cubarsi, Lamine Yamal, Fermin Lopez na Gavi.

Hata hivyo, taarifa kutoka kwa mwandishi maarufu wa habari za michezo wa Uingereza, Ben Jacobs, amesema kwa sasa Xavi hayupo kwenye hesabu za Xavi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img