MANCHESTER, Uingereza
KLABU ya Napoli imethibitisha kukwama katika mpango wake wa kumsajili kiungo wao wa mkopo kutoka Manchester United, Rasmus Hojlund.
Hojlund mwenye umri wa miaka 23, alitua kwa mkopo Napoli mwaka jana na klabu hiyo ya Italia inaruhusiwa kumbakiza kwa Pauni milioni 38.
Ripoti zinaeleza kuwa raia huyo wa Denmark ameshakubaliana na mabosi wa Napoli juu ya kubaki klabuni hapo.
Ikumbukwe, alisajiliwa na Man United mwaka 2023 akitokea Atalanta, dili hilo likigharimu kitita cha Pauni milioni 76.
Aliondoka Old Trafford akiwa amefunga mabao 26 pekee katika mechi 95 za mashindano mbalimbali, kabla ya kupelekwa Napoli kwa mkopo.


