18 C
New York

Parlour aishauri Arsenal kumsajili Alvarez

Published:

LONDON, Uingereza

MKONGWE wa Arsenal, Ray Parlour, ameishauri klabu hiyo kuharakisha usajili wa mshambuliaji wa kati wa Atletico Madrid, Julian Alvarez.

Parlour raia wa England, anaamini Alvarez ndiye anayepaswa kutua Emirates endapo Gabriel Jesus ataondoka mwishoni mwa msimu huu.

Jesus amekuwa akihusishwa na mpango wa kutimka Emirates, ambapo Juventus inatajwa kuitaka saini yake, pia ikielezwa kuwa huenda akarejea kwao, Brazil.

“(Gabriel) Jesus anaweza kuondoka Arsenal mwishoni mwa msimu huu, ana umri unaomtaka kucheza mara kwa mara,” amesema Parlour.

“(Julian) Alvarez utakuwa usajili mzuri kuziba pengo lake, kutokana na kasi na kile alichowahi kufanya alipokujwa Manchester City.”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img