9.2 C
New York

Nini chanzo UAE kujitoa OPEC? Ni ushindi kwa Rais Trump?

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

UMOJA wa Falme za Kiarabu (UAE) umetangaza kujitoa katika Umoja wa nchi zinazozalisha mafuta duniani (OPEC), hatua inayotafsiriwa kuwa ni ushindi mkubwa kwa Rais wa Marekani, Donald Trump.

UAE, moja ya nchi zinazozalisha na kuuza mafuta kwa wingi duniani, imekuwa mwanachama wa OPEC kwa miaka 60.

Hatua ya kujitoa imetajwa kuwa ni pigo kubwa kwa Umoja huo unaoongozwa na Saudi Arabia. UAE ni nchi ya tatu kwa uzalishaji mkubwa wa mafuta duniani.

Pia, UAE imejitoa wakati huu soko la mafuta duniani likiwa kwenye shinikizo kubwa la kupungua kwa ushambasaji wa nishati hiyo kutokana na mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati kati ya Iran na ushirikiano wa Marekani na Israel.

Wanaotafsiri hatua hiyo kuwa ni ushindi kwa Rais Trump wanasema kwa muda mrefu kiongozi huyo amekuwa havutiwi na uwepo wa OPEC.

Kwa madai kuwa wakati mwingine Umoja huo umekuwa ukipunguza uzalishaji kwa makusudi ili kujinufaisha na ubandaji wa bei ya mafuta katika soko la dunia.

Katika hatua nyingine, UAE kujitoa OPEC kunahusishwa na uhusiano uliyoyumba kati yake na Saudi Arabia.

Umoja huo ulioasisiwa na mataifa matano, ambayo ni Saudi Arabia, Iran, Iraq, Kuwait na Venezuela, unamiliki asilimia takribani 80 ya akiba ya mafuta duniani.

Mataifa hayo yalianzisha OPEC mwaka 1960, kabla ya Algeria, Equatorial Guinea, Gabon, Libya, Nigeria na DRC kujiunga hapo baadaye.

Kwa sasa, mgogoro unaofukuta Mashariki ya Kati unatajwa kuwagawa baadhi ya wanachama wa Umoja huo.

Hivi karibuni, Mashauri wa Diplomasia wa Rais wa UAE, Anwar Gargas, alizitupia lawama nchi za Kiarabu akisema hazikuonesha jitihada zozote za kuisaidia iliposhambuliwa na Israel.

Wakati huo huo, ipo dhana kuwa UAE inaona kufanya biashara ya kuuza mafuta nje ya Umoja wa OPEC kutaipa faida kubwa zaidi wakati huu bei ya nishati hiyo ikiwa imepanda duniani kote.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya soko la dunia, bei ya mafuta imefikia Dola 119.50 tangu kuanza kwa vita vya Iran dhidi ya mataifa mawili; Marekani na Israel.

Ikiwa nje ya masharti ya OPEC, UAE itaweza kuuza mafuta kwa kadiri itakavyotaka, kama ambavyo tayari imeahidi kuongeza mara dufu nishati hiyo katika soko la dunia.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img