KAMPALA, Uganda
SERIKALI ya Marekani imewahamishia nchini Uganda wahamiaji haramu nane, ukiwa ni utekelezaji wa mkataba uliosaniwa mwaka jana kati ya mataifa hayo.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda imethibitisha hilo, ikisema wahamiaji hao wamewasili Aprili 2, 2026 baada ya kesi zao kusikilizwa huko Marekani.
Uganda kupitia Wizara hiyo imedai kuwa Marekani ilisaini mkataba baada ya kuiona nchi yao kuwa ni sehemu salama kwa wahamiaji hao.
Hata hivyo, Chama cha Wanasheria cha Uganda kimelaani mpango huo na kusema Marekani imeigeuza nchi yao kuwa jalala la wahamiaji.
Aidha, Chama hicho kimeahidi kufungua kesi mahakamani ili kupinga mpango huo kisheria.


