18.1 C
New York

Ndege ya jeshi yapata ajali, 29 wafariki

Published:

MOSCOW, Urusi

WIZARA ya Ulinzi ya Urusi imethibitisha kifo cha watu 29 walilokuwamo kwenye ndege ya kijeshi iliyopata ajali mjini Crimea.

Ndege hiyo ya masafa ya kila siku aina ya An-26 imepata ajali baada ya kupoteza mawasiliano, kwa mujibu wa taarifa za Wizara hiyo.

Kwa kuwa ni ‘ishu’ ya mawasiliano, hakuna uhusiano wa kuanguka kwa ndege hiyo na vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine.

Kwa mujibu wa taarifa, ndege hiyo ya jeshi ilikuwa na abiria 23 na ilikuwa kwenye safari zake za Crimea, eneo ambalo Urusi ililiteka kutoka Ukraine mwaka 2014.

Kwa sasa, Kamati ya Uchunguzi ya Urusi imedai kuwa inaendelea kutafuta taarifa zaidi juu ya kilichotokea.

Kwa upande wake, Serikali ya Ukraine haijatoa taarifa yoyote kugusiana na ajali hiyo.

An-26 ni miongoni mwa ndege kongwe za kijeshi, ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo mikubwa, kusafiri umbali wa kawaida, na idadi ndogo ya abiria.

Inafahamika wazi kuwa ndege hizo huzalishwa na kampuni maarufu ya Ukraine inavyofahamika kwa jina la Antonov.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img