LOS ANGELES, Marekani
STAA wa mchezo wa gofu, Tiger Woods, amerejea uraiani tangu alipokamatwa kwa kesi ya kuendesha gari akiwa amelewa pombe.
Woods, bingwa wa dunia mara 15, aligundulika kuwa alikuwa amelewa baada ya gari lake kupata ajali mjini Florida.
Ripoti zinaeleza kuwa ajali hiyo ilitokana na jaribio lake la kukwepa gari la takataka akiwa kwenye mwendo mkali.
Baada ya kukamatwa, Woods ambaye hata hivyo hakupata majeraha katika ajali hiyo, aligoma kufanyiwa vipimo vya haja ndogo.
Tangu alipokamatwa, Woods mwenye umri wa miaka 50 amekuwa mahabusu kwa siku nane na sasa ameachiwa kwa dhamana..


