TEHRAN, Iran
KIKUNDI kinachohusishwa na ugaidi cha Houthis cha nchini Yemen kimeanzisha mashambulizi dhidi ya Israel.
Siasa za kimataifa zinakitaja kikundi hicho kupata ufadhili wa fedha, silaha na mbinu kutoka kwa Iran.
Hii ni mara ya kwanza kwa Houthis kuingia kazini kuisaidia Iran tangu Israel ilipoungana na Marekani kuishambulia nchi hiyo ya Kiarabu.
Katika mashambulizi yake, Houthis wamesema wamelenga maeneo ya kijeshi nchini Israel.
Kwa upande mwingine, kuingia kwa Kundi hilo kumeibua hofu kwamba huenda vita hivyo vikachukua muda mrefu zaidi.
Wakati mashambulizi yakiendelea, Rais wa Marekani, Donald Trump, amedai kuwa kuna dalili nzuri za kumalizika kwa vita hivyo.
Kwa mujibu wake, wawakilishi wa Marekani wanatarajiwa kukutana, kukaa mezani na kuzungumza na viongozi wa Iran.
Hata hivyo, tayari Wizara ya Ulinzi ya Iran ilishaweka wazi kuwa haiko tayari kufanya mazungumzo ya amani na Marekani wala Israel.


