22.6 C
New York

Rais Zimbabwe aachia wafungwa 4,000

Published:

HARARE, Zimbabwe

RAIS wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, ametangaza msamaha wa wafungwa takribani 4,000, ikiwa ni hatua ya kupunguza msongamano magerezani.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa kile kilichoahidiwa na Baraza la Mawaziri mwezi uliopita, wakati wa kupitisha mabadiliko ya Katiba inayoweza kumbakiza madarakani Rais Mnangagwa hadi mwaka 2030.

Taarifa zinaeleza kuwa jumla ya wafungwa waliorejea uraiani ni 4,305, wakiwamo wanawake 223.

Miongoni mwao ni kijana mwenye umri wa miaka 23, Tendai Chitsika, ambaye amekuwa gerezani kwa miezi sita kwa makosa ya wizi.

“Ni somo kwangu. Nimekuwa mtu wa tofauti sasa. Naahidi kubadilika na pia napenda kumshukuru Rais kwa nafasi hii,” amesema.

Related articles

Recent articles