TEHRAN, Iran
WAPIGANAJI wa Kundi linalohusishwa na ugaidi la Hezbollah nchini Lebabon wamerushiana risasi na makombora na wanajeshi wa Israel.
Hiyo ni baada ya Israel na Marekani kuanzisha mashambulizi makubwa ya kivita dhidi ya Iran inayotajwa kuifadhili Hezbollah.
Taarifa za awali zilizotolewa na Marekani zinadai kuwa wanajeshi wake watatu wameuawa katika mapambano yao dhidi ya Kundi hilo.
Hezbollah wameingia kuishambulia Israel zikiwa ni saa chache baada ya vyombo vya habari vya kimataifa kuripoti kuwa Rais wa zamani wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, ameuawa.
Kabla ya taarifa hiyo, Marekani kupitia Rais Donald Trump ilitangaza kumuua aliyekuwa kiongozi Mkuu wa Taifa hilo, Ali Khamenei.
Katika siku chache tangu Marekani na Israel zilipoungana kuishambulia Iran, athari zake za kiuchumi zimeanza kuonekana, ikiwa ni pamoja na kupanda kwa bei ya mafuta duniani na kukwama kwa safari za ndege za kimataifa.


