TEHRAN, Iran
ALIYEWAHI kuwa Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, ameuawa kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na vikosi vya ushirika kati Marekani na Israel.
Profesa Ahmadinejad alikuwa Rais wa Iran kuanzia mwaka 2005 hadi 2013, na baada ya kustaafu alirudi kufundisha katika Chuo Kikuu cha Tehran, ambapo hadi umauti ulipomkuta alikuwa mkufunzi Idara ya Fizikia.
Kifo cha Ahmadinejad kinafuatia orodha ya vifo vya viongozi waandamizi wa Iran akiwemo Ayatollah Ali Khamenei aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa taifa hilo, na Said Abdulrahim Mousavi aliyekuwa Mkuu wa Majeshi.
Wengine waliouawa hadi sasa ni pamoja na Aziz Nasirzadeh – Waziri wa Ulinzi, Jenerali Mohammad Pakpour – Mkuu wa Kamandi ya nchi kavu, Jenerali Ali Shamkhani – Mkuu wa Usalama wa Taifa na mshauri wa Ayatollah Khamenei, Jenerali Hossein Jabal Amelian – Mkuu wa Taasisi ya Utafiti Jeshini, na Jenerali Mohammad Shirazi – Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi wa Ayatollah Khamenei.


